HALAL CERTIFICATION

MRADI WA UTOAJI WA CHETI CHA HALAL KWA WAUZA NYAMA WOTE NCHINI TANZANIA

1. JINA LA MRADI

Mradi wa Usajili na Utoaji wa Cheti cha Halal kwa Wauza Nyama Nchini Tanzania

2. MWANZILISHI/MRATIBU

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)

3. MAELEZO YA MRADI

Mradi huu unalenga kuanzisha mfumo rasmi wa usajili, ukaguzi na utoaji wa vyeti vya Halal kwa wauza nyama nchini kote. Lengo ni kuhakikisha kwamba nyama inayouzwa inazingatia misingi ya Kiislamu katika uchinjaji, uhifadhi, usafishaji na usambazaji.

4. LENGO KUU LA MRADI

Kuhakikisha wauzaji wote wa nyama nchini wanazingatia kanuni na masharti ya Halal, kwa manufaa ya Waislamu na jamii kwa ujumla.

5. MALENGO MAHSUSI

  • Kutoa elimu kwa wauza nyama kuhusu taratibu za Halal.
  • Kufanya ukaguzi wa maduka ya nyama na machinjio.
  • Kutoa vyeti vya Halal kwa wale wanaokidhi vigezo.
  • Kuanzisha utaratibu wa usimamizi wa ubora na ufuatiliaji wa nyama Halal.
  • Kukuza imani ya walaji Waislamu kwa bidhaa wanazonunua.

6. WALENGWA WA MRADI

  • Wauza nyama wote nchini (maduka ya nyama, machinjio, wazalishaji wa nyama ya kusindika).
  • Wateja wa nyama (hasa Waislamu).
  • Serikali za mitaa na taasisi za afya.

7. MAENEO YA UTEKELEZAJI

Mradi utatekelezwa nchi nzima, ukianza na mikoa mikuu kabla ya kuenea hadi wilaya zote.

8. MIKAKATI YA UTEKELEZAJI

  • Awamu ya Kwanza: Uhamasishaji na elimu kwa wauza nyama.
  • Awamu ya Pili: Ukaguzi wa maduka ya nyama na machinjio.
  • Awamu ya Tatu: Utoaji wa vyeti vya Halal kwa wanaokidhi vigezo.
  • Awamu ya Nne: Ufuatiliaji na ukaguzi wa mara kwa mara.
  • Awamu ya Tano: Uundaji wa mfumo wa kidigitali wa kuhifadhi taarifa za walioidhinishwa.

9. FAIDA ZA MRADI

  • Kuimarisha imani ya walaji Waislamu kwa nyama wanayonunua.
  • Kuboresha viwango vya usafi na usalama wa vyakula.
  • Kupunguza migogoro ya kisheria na kijamii kuhusu nyama zisizo Halal.
  • Kutoa ajira kwa wakaguzi na wahamasishaji.
  • Kuongeza hadhi ya wauza nyama wanaofuata taratibu za Halal.

10. WADAU WA MRADI

  • BAKWATA
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Serikali za Mitaa
  • Jumuiya za Waislamu
  • Wadau wa biashara ya nyama

11. MUDA WA MRADI

Mradi huu ni endelevu